Mtoto mdogo wa umri wa miezi sita na kuendelea anaposhindwa kuongezeka uzito na maendeleo ya ukuaji wake kudhorota ni ishara ya kutosha kuwa afya yake si sawa kwa ujumla.
Katika kipengele hiki ntazungumzia sababu zinazochangia ukosefu wa afya bora kwa watoto wadogo kuanzia umri wa miezi sita na kuendelea kama ifuatavyo:
Ulishaji hafifu wa vyakula vyenye virutubisho muhimu, kuna wakati mama au mlezi wa familia anashindwa kumpa mtoto vyakula vyenye virutubisho aina fulani, hivyo mtoto anakosa virutubisho hivyo na kufanya afya yake kudhorota.
Umaskini, baadhi ya familia zinashindwa kuwapa watoto vyakula vya kutosha vyenye mchanganyiko wa virutubisho kutoka katika baadhi ya makundi ya vyakula kama vyakula vya protini, vitamini na madini kutokana kushindwa kumudu gharama ya kununua vyakula hivyo.
Vyakula venye protini kama nyama, samaki, kuku, maziwa, vinapatika kwa gharama kubwa hivyo familia nyingi zinashindwa kumudu gharama hizo na kushindwa kuwapa watoto virutubisho vya protini vya kutosha kujenga afya.
Watoto kupewa chakula kidogo, baadhi ya watoto wanakuwa na matatizo ya kula chakula cha kutosha hii inaweza kusababisha kudhorota kwa ukuaji wake.
Hali ya kitabibu ambayo inaweza kumfanya mtoto akawa anapata tabu katia kumeza chakula na kumfanya mtoto kutopenda kula chakula kutokana aina na radha ya chakula.
Matatizo ya kiafya yenye kuathiri mfumo wa umengenywaji chakula, tatizo la mfumo wa umengenywaji unaweza kufanya mtoto akashindwa kuongezeka uzito.
Kuathiriwa na ugonjwa, mwili wa mtoto unatumia virutubisho vingi kupambana na magonjwa mtoto ambaye hajisikii vizuri anaweza kula kidogo isivyo kawaida.
0 Comments