SBL yaja na kampeni kuwalinda Wanafunzi
UNYWAJI wa Pombe katika umri mdogo limekuwa tatizo kubwa katika jamii. Nchini Tanzania, zipo mila ambazo bado watoto wadogo wamekuwa wakishirikishwa katika hafla ambazo zinashirikisha pombe, ingawaje kuna sheria ambazo zinazuia watoto kuingia kwenye vilabu vya Pombe.
Kuna kampeni mbalimbali hata hivyo zimefanywa kuhakikisha kwamba watoto wadogo hawaruhusiwi kunywa pombe, na wadau wanaozalisha pombe wamekuwa wakiwema mpaka matangazo kwenye bidhaa wanazozalisha kwamba watoto chini ya umri wa miaka 18 hawaruhusiwi kunywa Pombe. Pamoja na matangazo hayo, bado kumekuwa na tabia ambayo inaweza kuathiri makuzi na maendeleo ya watoto kutokana na unywaji wa Pombe. Katika hatua ya kufurahisha,
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imeungana na wadau wa elimu wa mkoani Tanga, kupambana na unywaji pombe kwa watu wenye umri mdogo ili kudhibiti tabia ya unywaji pombe miongoni mwa wanafunzi wa shule. SBL imeshirikiana na Afisa Elimu Taaluma Sekondari wa Jiji la Tanga, Maurus
Ndunguru na Afisa Maendeleo wa Jiji la Tanga na Mratibu Mashirika ya Kijamii Naetwa Kilango, kusambaza elimu ya kuepuka matumizi ya pombe kwa wanafunzi katika halfa maalum iliyofanyika katika shule ya sekondari Nguvumali.
Kampeni hiyo iliyopewa jina la SMASHED, ni kampeni ya kupambana na unywaji wa pombe ya SBL, inayotumia michezo ya kuigiza ya jukwaani inayowapa uezofu wa kipekee na kusisimua. Kama nilivyosema hapo juu,
Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zenye kundi la watu wenye umri mdogo wa wanaotumia pombe na tabia hii imeharibu na kuondoa misingi imara ya watoto hao katika mambo mbalimbali ikiwemo makuzi binafsi na kielimu.
Utafiti uliofanywa mwaka 2019 katika mikoa ya Mwanza na Kilimanjaro ulibaini kuwepo kwa mwenendo wa matumizi ya pombe miongoni mwa wanafunzi wa shule za sekondari wenye umri wa miaka 15 na zaidi ni kutoka asilimia 12.9 miongoni mwa wasichana mkoani Mwanza hadi asilimia 63.9 miongoni mwa wavulana mkoani Kilimanjaro.
Kwa hiyo, SMASHED hufanyika mashuleni na huelimisha wanafunzi wa sekondari kuhusu madhara ya matumizi ya pombe katika umri mdogo, kwa kuwashauri kujiepusha na matumizi ya pombe kabla ya kukomaa.
Programu hii inachanganya matumizi ya maonyesho ya maigizo na ushiriki wa wanafunzi katika mazingira ya motisha ya kujifunza ili kuwapa ukweli, ujuzi na ujasiri wa kufanya uchaguzi wa kuwajibika na kuendeleza mitazamo ya uwajibikaji katika masuala yanayohusiana na afya.
Afisa Elimu Taaluma Sekondari wa Jiji la Tanga, Maurus Ndunguru, alipongeza SBL kwa kampeni ya SMASHED na kutoa mapendekezo zaidi. “Kampeni hii itasaidia sana vijana wetu wa shule, hasa katika shule hizi tano mlizozifikia, maana wanafunzi wamekuwa wakipata changamoto za ulevi. Nashauri pia, kampeni hii iweze pita katika shule zote mkoani Tanga” Alisema Ndunguru.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Umma wa SBL alisema: "SMASHED inatoa mafunzo muhimu juu ya athari mbaya za unywaji pombe katika umri mdogo kwa vijana na jamii, kwa makusudi mazima ya kulinda ndoto na ustawi wa vijana, ili kuhakikisha wanafanikiwa katika jitihada zao".
Wanyancha alisema mpango huo umetekelezwa nchi nzima tokea Oktoba 2022 kwa awamu, kuanzia Dar es Salaam na kuhamia mkoani Tanga. Zaidi ya wanafunzi 15,000 wamefikiwa nampango huo katika mikoa hiyo miwili.
Afisa Maendeleo wa Jiji la Tanga na Mratibu Mashirika ya Kijamii Naetwa Kilango amefurahishwa na mbinu za kibunifu za utoaji elimu kwa vijana na kuwaomba wadau wenginekubuni miradi ya kulinda ndoto za wanafunzi.
"Ahsanteni Serengeti Breweries kwa ushirikiano wenu katika kuwaasa vijana hawa na kuwapambinu za kulinda kesho yao. Kwa kweli vitendo vya matumizi ya pombe katika umri mdogo ni lazima vipigwe vita na SMASHED ni jukwaa muhimu sana", alisema Kilango. Kwa upande mwingine, Ocheck Msuva mwanzilishi wa asasi ya kiraia ya vijana,
Bridge for Change inayotumia sanaa ya maigizo ya jukwaani kufikisha ujumbe, amesema SBL inawapa vijana nafasi ya kupanga kesho yao wakiwa na maarifa ya kutosha kufanya maamuzi makini. “Ikiwa vijana watakuwa na uelewa, maarifa na elimu juu ya madhara ya urahibu wa vilevi ni stahiki kabisa watakuwa na nafasi ya kufanya maamuzi sahihi ambayo ni kiini cha kuelekea katika njia ya mafanikio.” Alisema Ocheck.
Kampeni hiyo ya SMASHED imekelezwa ndani ya shule tano za sekondari jijini Tanga, nazo ni: Nguvumali, Kihere, Toledo, Masechu na Mnyanjari sekondari. Kampeni hii imebeba misingi mizuri kwa ajili ya watoto wetu, na Serengeti Breweries wameonesha kujali watoto wetu na kampeni hii inaonesha kwamba licha ya kuzalisha pombe, lakini SBL ni walinzi wazuri wa watoto wetu pia.
Kampeni hii inaweza kuendelezwa kwa kufanyika kwenye mikoa iliyobobea kwa unywaji wa pombe kwa umri huo mdogo, lakini pia isambazwe kwenye vyombo vya habari na pia kutetea sheria zinazozuia watoto kuingia kwenye maeneo ambako pombe inauzwa!
0 Comments