Kama tunavyofahamu kuwa afya ni hali ya kuwa sawa kimwili, kifikra na kutokuwa na maradhi au kasoro ya aina yoyote pamoja na kutobughudhiwa na hali ya aina yoyote.

Kwa mtoto mdogo kuanzia miezi sita na kuendelea anapokuwa na ugonjwa au kasoro ya aina yoyote ya kimwili hali hiyo inachukuliwa kuwa afya yake kwa ujumla haiko sawa.

Katika kipengele hiki ntazungumzia baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na upungufu wa lishe kwa mtoto (malnutrition), na hivyo kupelekea mtoto kukosa afya bora.

Baadhi ya magonjwa yanayotokana na upungufu wa lishe bora kwa watoto ni pamoja na ugonjwa wa surua, kuharisha, upofu, nimonia, kwashoikor na upungufu wa vitamini A mwilini.

Magonjwa yanayotokana na upungufu wa vitamini A ni kama(Xerophthlmia), husababisha upofu wa macho, ukavu kwenye mwili na kupelekea maendeleo hafifi ya ukuaji wa mwili wa mtoto.

Ugonjwa wa Beri-beri, ugonjwa huletwa na ukosefu wa vitamini B1 mwilini husababisha matatizo ya moyo, utengenezwaji wa neva, na kuharibu mchakato mzima wa uratibiwaji wa misuli ya mwili.

Rickets (matege) ni ugonjwa unaosababishwa na ukosefu wa vitamini D mwilini husababisha mifupa kuwa dhaifu na maendeleo hafifu ya ukuaji wa mwili wa mtoto na miguu kuwa na matege.

Goiter (kuvimba shingo) ni ugonjwa unaosababishwa na ukosefu wa madini ya iodine mwilini, husababisha kuvimba shingo na kuleta maendeleo hafifu ya ukuaji wa mwili wa mtoto mdogo kutokana na ukosefu wa virutubisho.