Ni muhimu sana kwa mama au mlezi wa mtoto kufahamu kwa kina baadhi ya mambo ya msingi yanayoashiria kuwa mtoto mdogo anaendelea vizuri kiafya.

Katika kipengele hiki ntazungumzia kwa kina jinsi ya kujua kama mtoto anaendelea vizuri kimwili, kifikra, kihisia na kisaikolojia katika maendeleo ya ukuaji wake.

Watoto wanatofautiana katika hatua za ukuaji lakini mambo yafuatayo yanaweza kukuongoza katika kutambua kuwa mtoto anaendelea vizuri kiafya.

Kutaka kunyonya kila wakati, watoto wanazaliwa na asili ya kunyonya na kuweka vitu mdomoni, hivyo kitendo cha mtoto kuhitaji mara kwa mara kutaka kunyonya ziwa la mama kinaashiria kuwa ana hamu ya kula na mfumo wake mzima umengenywaji chakula uko sawa.

Kupata choo mara nne hadi sita kwa siku, ukimbadilisha mtoto nepi mara nne hadi sita kwa siku sio tu ana kula vizuri bali hana tatizo la upungufu wa maji mwilini (hydrated) yuko vizuri.

Iwapo utakuwa ukimbadilisha nepi mtoto mara chache chini ya kiwango kinachopendekezwa hatatoweza kuongezeka uzito na hii ni dalili ya kutopata lishe ya kutosha.

Kuhamaki au kuonesha shauku ya milio mbalimbali, kama luninga,redio au midori watoto wana uwezo wa kusikia tangu wakiwa tumboni mwa mama, ukiona mwanao ana shauku anaposikia milio mbalimbali ni dalili ya maendeleo mazuri ya ukuaji wake wa kifikra.

Kuongezeka uzito na kimo, watoto wanakuwa haraka katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo anatakiwa aongezeke uzito mara mbili ya uzito wa kuzaliwa kwa miezi mitano na mara tatu ndani ya mwaka.

Kuona vizuri vitu kama rangi, mijongeo (movements), mtoto ana uwezo wa kuona umbali wa nchi 8 hadi 12, sawa na umbali anapokuwa amebebwa akinyonyeshwa ziwa la mama akimtazama vizuri mama ni ishara kuwa uwezo wake wa kuona uko sawa na maendeleo ya akili yake yako sawa.

Kupata usingizi vizuri, usingizi ni muhimu sana kwa maendeleo ya afya ya mtoto kama mtoto wako analala vizuri inaashiria kuwa yuko vizuri hana kero inayomsumbua na mwenye furaha.

Inashauriwa kama kutakuwa na kuchelewa katika maendeleo ya afya ya mtoto muone daktari kuchunguza sababu na kukushauri hatua sahihi za kuchukua kusaidia afya ya mtoto wako.