Jengo la Ghorofa Moja 


Ujenzi wa nyumba na maghorofa katika jiji la Dar es salaam, umekuwa ukifanywa kiholela kwa kukiuka taratibu za ujenzi zinazosimamiwa na Bodi ya Wakandarasi Nchini (CRB),

Uchunguzi uliofanywa na Morningstar Post umebaini kuwa majengo mengi yanayojengwa yanashindwa kutekeleza sheria za ujenzi kwa wakati na kwa utaratibu unaotakiwa.

Katika maeneo mengi ambayo tumetembelea kushuhudia majengo mengi yakijengwa huku kukiwa hakuna bango au nembo ya CRB kuonesha kuwa mradi huo umesajiliwa kwenye bodi CRB na wahusika ni watu sahihi wanaofanya ujenzi huo.

Baadhi ya wakandarasi waliohojiwa walikiri kuchelewa kuweka bango na nembo ya CRB wakieleza kuwa wameshakamilisha usajili lakini hawajaweka nembo.

Akizungumza na Morningstar Blog, Msajili wa CRB, Ruben Nkoli, alisema utaratibu wa kusajili mradi kwa wakandarasi uko mtandaoni kwa makampuni yatakayoshindwa kufanya hiyo wakiwabaini watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Amewataka wakandarasi wote kuhakikisha wanasajili miradi kwa wakati na kuanza ujenzi mara tu usajili unapokamilika ikiwa pamoja na kufuata sheria zote za ujenzi katika mradi husika.