Katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo maziwa ya mama yanavirutubisho vyote muhimu kwa ajili ya kujenga afya ya mtoto, hivyo ni muhimu sana kunyonyesha mtoto wako vizuri katika kipindi hicho.
Hata hivyo unyonyeshaji wa maziwa ya mama hauwezi kuwezekana kwa wanawake wote kutokana na sababu mbalimbali kama mtindo wa maisha na hali fulani ya matibabu.
Hatua ya kwanza ya kumsaidia mtoto anayekosa maziwa ya mama ni kumpa maziwa ya fomula au maziwa ya kopo kwa kawaida yanatengenezwa kwa maziwa ya ngombe yanaandaliwa kwa kuyafanya yawe yenye kukidhi na bora kwa watoto.
Kuna aiana nyingi za maziwa haya kwenye maduka unatakiwa kuangalia lebo vizuri kuhakikisha unanunua maziwa mazuri kwa mtoto wako.
Maziwa haya yanakuja aina mbili kuna maziwa ya unga na ya maji ambayo hayana usumbufu katika kutumia ingawa ni gharama kuliko ya unga na unapoyafungua unatakiwa kuyatumia ndani muda mfupi.
Maziwa haya ya kopo yana virutubisho vyote kwa ajili ya kumfanya kuwa vizuri katika maendeleo yake ya ukuaji, hata hivyo faida yake hayawezi kuwa sana na maziwa ya mama, hayawezi kumlinda mtoto wako na kuathiriwa na maradhi.
Hata hivyo sio kila maziwa ni salama kwa kumpa mtoto wako usimpe mtoto maziwa kama 'condensed milk', 'evaporated milk', 'drie milk' (ni maziwa ya ngombe yaliondolewa maji), maziwa mbuzi or kondoo (lakini ni sawa kutumiwa yanapopikwa kwa ajili ya mtoto pamoja na kufanyiwa kuliwa bakteri bila kuathiri virutubisho (pasteurised)
0 Comments