Mama au mlezi wa familia ni vyema akaelewa vizuri kwa kina maana ya afya ya mtoto kuanzia umri wa miezi sita na kuendelea na jinsi ya kumsaidia mtoto kujenga afya bora.
Katika kipengele hiki ntazungumzia zaidi maana halisi ya afya kwa mtoto tangu kuzaliwa na kuendelea.
Shirika la Afya Duniani (WHO), limeeleza maana ya afya kuwa ni hali ya kuwa sawa kimwili, kifikra na kutokuwa na maradhi au kasoro ya aina yoyote pamoja na kuwa katika hali ya kutobughudhiwa na fikra, hisia, maradhi au jamii inamyozunguka.
Kutokuwa na maradhi au kasoro ya aina yoyote kimwili, kifikra na hata kisaikolojia. Hali ambayo inampa mtu kushiriki kikamilifu katika harakati zote za maisha ya kila siku, hali ya uwiano sawa wa mtu na jamii yake na mazingira.
Afya inaonekana ni rasilimali muhimu inayosaidia kushughulikia maisha yetu ya kila siku
Kwa ujumla afya ni nadharia pana sana inayotafsiri rasilimali za mtu kijamii pamoja na uwezo wa mwili katika kushugulikia maisha.
Hali ya kuwa sawa kimwili, kifikra na kiroho, kuwa huru na maradhi yanayoshambulia miili yetu maumivu ya aina yoyote ya kifikra na kimwili.
Hali ya mwili wa mototo uliosawa kwa ujumla hali ambayo anaendelea vizuri katika maendeleo ya ukuaji wake bila kasoro ya aina yoyote.
0 Comments