Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Newala Mkoa Mtwara, Innocent Sotter, amechukizwa na vitendo vya ushoga ambavyo vimekuwa vikishamiri nchini.
Hali hiyo imedhirika baada ya kumuhukumu kifungo cha miaka 30 jela Selemani Mustafa maarufu kama Sele makazi wa wilaya hiyo baada ya kukiri kujihusisha na vitendo vya ushoga.
Mshitakiwa huyo alikiri mwenyewe baada ya kusomewa mashtaka kuwa amekuwa akijuhusisha na vitendo vya ushoga na kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile na wanaume mbalimbali kwa nyakati tofauti.
Kitendo hicho kilimchukiza hakimu Sotter na kuwageukia upande wa mashtaka ambao uliomba mshtakiwa adhibiwe kwa mujibu wa sheria.
Upande wa mashtaka ulimuomba hakimu hiyo kutoa adhabu kwa mujibu wa kifungu cha 154 cha kanuni ya adhabu ili iwe fundisho kwake na onyo kwa jamii nzima kwa kuwa vitendo vya ushoga vimeongezeka na kusababisha mmongonyoko wa maadili katika jamii yetu.
Hakimu hiyo hakupepesa macho kutoa adhabu hiyo baada ya mstakiwa huyo kukiri kutenda kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile na wanaume mbalimbali kwa nyakati tofauti.
Licha ya mtuhumiwa huyo kujitetea kuwa anaomba apunguziwe adhabu kwa kuwa atajirekebisha, hakimu huyo alimuhukumu miaka 30 jela kwa kukosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na kifungu cha 154 (1) (c) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo ya mwaka 2022.
Hatua ya hakimu huyo kutoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela imewatahadharisha baadhi
ya watu ambao wamekuwa wakijitangaza kuwa ni mashoga kujihadhari kwa kuwa ushoga haukubaliki kwa mujibu wa sheria za nchi.
0 Comments