Halmashauri ya jiji la Dar es salaam, imeshindwa kusimamia sheria ya mipango miji inayoelekeza uendelezaji wa majengo ya juu katika maeneo ya katikati ya jiji la Dar es salaam.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na blog hii umebaini kuwa majengo mengi ya chini yasiyotakiwa kujengwa yanashamiri kujengwa katikati ya jiji hususani katika maeneo ya Kariakoo.
Katika barabara ya Msimbazi maeneo ya kituo cha mafuta cha Big Bon, kumejengwa jengo la chini ambalo hapo awali halikuwepo kinyume na sheria ya mipango miji inayoelekeza halmashauri kusimamia ujenzi wa majengo ya juu katikati ya jiji kukabiliana na ongezeko la ujenzi holela.
Akizungumza na Morningstar Post, Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam, Bw Amani Mafuru, alishindwa kutoa maelezo kuhusu jengo hilo, lililojengwa maeneo ya Msimbazi kwenye kituo cha mafuta cha Big Bon.
"Mimi ni Mkurugenzi sihusiki na mambo yanayofanyika kwenye field, hapa kwangu kuna kuja mafaili zaidi ya mia sita kila siku ntafahamu vipi mambo yanayofanyika huko nje," alisema.
Bw. Amani alisema hapaswi kulaumiwa wala kutuhumiwa kwa makosa yanayofanywa na watendaji wake wa chini kama kuna makosa yoyote yanafanyika mkurugenzi hapaswi kutuhumiwa yeye bali inapaswa kuhushwa ni ofisi yake.
Akaongeza kuwa kuhusu ufafanuzi wa jengo hilo lililojengwa kwenye kituo cha mafuta cha BigBon atafuatilia kwa watendaji wake wa chini yake na kutoa ufafanuzi kuhusu jengo hilo baadae.
Akasisitiza zaidi kuwa yeye hapaswi kutuhumiwa kwa makosa yanayofanywa na watendaji wake wa chini, malalamiko na tuhuma zote zinapaswa kuelekezwa kwenye ofisi ya mkurugenzi na sio mkurugenzi.
Mkurugezi alitoa ufafanuzi huo kufuatia maswali yalioelekezwa kwake na Morningstar Post yakimtuhumu mkurugenzi na injini wa jiji kuhusika kwa uvunjifu wa sheria ya mipango miji kwa kuruhusu majengo ya chini kuendelea kujengwa katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Uchunguzi wa Morningstar Post umebaini kuwa majengo mengi ya chini yanayojengwa katikati ya jiji la Dar es salaam hayana vibali au yanakuwa yanatumia vibali vya ukarabati vinavyotolewa na halmashauri na kuanzisha ujenzi mpya.Hali ambayo inashindwa kusimamiwa na watendaji wa halmashauri kuanzia ngazi ya kata.
Kwa mujibu wa sheri ya mipango miji inaelekeza wazi kutotolewa kwa vibali vipya vya ujenzi wa majengo ya chini katika maeno ya katikati ya jiji la Dar esa Salaam badala yake jiji liendelezwe kwa ujenzi wa majengo ya juu.
Kutokana na uhitaji mkubwa wa maduka ya biashara wamiliki wengi wa nyumba hususani katika maeneo ya karikaoo wanashindwa kujenga majengo ya juu badala yake wanatumia vibali vya ukarabati kujenga fremu za maduka.
0 Comments