Hali ya demokrasia ya vyama vya siasa nchini Tanzania, inaeendelea kuimarika na kuleta tija kwa maendeleo ya siasa na uchumi wa nchi kufuatia kupigwa marufuku kwa zuio la vyama vya siasa kwa miaka sita.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuonesha ushirikiano wa kisiasa nchini kwa kukubali mwaliko wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Marchi 8, mwaka huu katika kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani.
Hatua hiyo ya kukubali mwaliko huo si tu inaendeleza ushirikiano wa vyama vya siasa bali inaimarisha demokrasia nchini na kuendelea kudumisha amani na utulivu wa kisisa nchini.
Chama cha ACT wazalendo kimempongeza sana Rais Samia kwa kukubali mwaliko wa Bawacha kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo kwa kuwa inaonesha kuwa ana nia njema ya Rais Samia katika kuimarisha demeokrasia chini iliyopotea kwa miaka sita ya marufuku ya kufanya mikutano ya kisiasa.
Rais Samia katika mkutano wake na vyama vya siasa nchini hivi karibuni alisema anakusudia kuanza kwa mchakato wa marekebisho ya katiba mpya, au katiba ya warioba.
"Serikali inadhamiria kukwamua mchakato wa marekebisho ya katiba, kwa jinsi tutakavokuja kuelewana huko mbele’, wengine wanasema tuanze na katiba ya warioba, wengine tuanze na katiba pendekezwa, lakini kuna mambo ya ulimwengu yamebadilika", alisema Rais Samia.
Mbali na hilo Rais Samia hatua yake ya kuondoa zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, lililodumu kwa zaidi ya miaka 7, tangu mwaka 2015, kumeleta mahusiano ya wananchi na wanachama wa vyama mbalimbali.
Hatua hiyo imewafanya wanasiasa kuanza kuonesha siasa za ushirikiano kwa kupongeza mambo ambayo yamekuwa yakifanywa na serikali tofauti na ilivyokuwa huko nyuma ambapo vyama vya siasa vilikuwa hakuna jambo lolote lililokuwa wanaunga mkono serikali ya CCM.
Wapinzani huko nyuma walikuwa hawaungi mkono jambo lolote la serikali hata kama ni jambo zuri limefanywa na serikali, tofauti na ilivyokuwa hivi sasa wapinzani wanakosoa serikali na kuipongeza kwa mazuri ya serikali.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwahi kuwaasa wanachama wa chama chake kutojenga chuki kwa wanachama wa CCM kwa yale yaliokuwa yanatokea huko nyuma.
Kualikwa kwa Rais Samia katika mkutano wa Bawacha ni ishara kuwa huu ni mwendelezo wa kuonesha ushirikiano wa serikali na vyama vya siasa, licha ya kuwa mkuutano huu umeandaliwa na wanawake kwa maadhimisho ya siku ya wanawake, lakini una sura ya kisiasa kwakuwa unahusu wanawake wa chama cha CHADEMA.
Vyama vya upinzani hususani chama cha Chadema vinaendelea kufanya mikutano ya kisiasa na kuzungumza na wananchi hali ambayo huko nyuma ilikuwa ni nadra, hatua hii ni ya kupongezwa kwa Rais Samia ambaye ni mwenyekiti wa CCM taifa kuleta uongozi wa kidemokrasia nchini.
0766600909
0 Comments