0744 499 499

Kampuni ya Sinota Group Indutries Ltd, inayoendesha kiwanda cha kushona mapazi kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam, kimeshindwa kuwakatia wafanyakazi wake uanachama wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF).

Kampuni hiyo inayoendeshwa na raia wa China, kwa miaka mingi nchini, ina zaidi ya wafanyakazi 30, lakini hakuna hata mmoja aliyekuwa mwanachama wa WCF.

Uchunguzi wa Morningstar Post, umebaini kuwa kampuni hiyo, inawafanyakazi 20 waliojiliwa na wengine ni vibarua lakini kati ya waliojiliwa hakuna hata mmoja aliyekuwa mwanachama wa WCF kinyume na sheria za kazi.

Akizungumza na mwandishi wa Morningstar Post, Meneja Rasilimali Watu, aliyejitambulisha kwa jina moja la Latifa, alikiri kutokufahamu jambo lolote kuhusiana na WCF.

Hata hivyo, akaelekeza mwandishi wa habari hizi kuwasilina na Mkalimani wao, ambaye alijitambusha kwa jina  moja la Karimu, alikiri kuwa kampuni hiyo haijawaandikisha wafanyakazi wake na mfuko huo wa fidia wa wafanyakazi WCF.

Akaongeza kuwa kampuni hiyo iko mbio kufuatilia suala hilo, licha ya kuwa ni miaka mingi imekuwa ikifanya kazi za kushona mapazia hapa nchini.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Morningstar Post, pia kampuni hiyo ya SINOTA inaendesha kiwanda hicho huku leseni yake ya biashara ya ghala (Gowdown), iliyotolewa na Manispaa ya Temeke ikiwa imekwisha muda wake tangu mwezi machi mwaka huu.

Pia kampuni hiyo inaendesha kiwanda hicho kwa leseni ya muda (temporary licence), kwa zaidi ya miaka saba.

Akijibu hoja ya kutokuwa na leseni Karimu alionesha kutokujua lolote licha ya uongozi wa kampuni hiyo kumwelekeza kwa waandishi kama msemaji wa kampuni.

Awali akizungumza na waandishi wa habari hizi, kiwandani hapo kunakozalishwa mapazia, Afisa Mwandamizi wa kampuni hiyo ambaye ni raia wa China aliyejitambulisha kwa jina moja la Chimei hakuweza kueleza lolote kutokana na kutokujua lugha ya kiswahili na Kingereza badala yake akaelekeza kuzungumza na meneja wake.

Akizungumza na Mornginstar Post, Meneja wa kampuni hiyo, Bi Halima Nasoro alisema hafahamu lolote kuhusu WCF na wafanyakazi waliojiliwa ni 20 na hawana uanachama wa WCF kwa muda mrefu.

Pia, Bi Halima alisema kuwa mambo mengine hawezi kuyaeleza na kuomba waandishi kuzunguza na Meneja Rasilimali Watu, Bi. Latifa.

Juhudi za kuwapata wahusika wa Manispaa ya Temeke idara ya biashara na uongozi wa WCF pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara hazikuweza kufanikiwa mara moja hivyo tutaendelea kufuatilia.