Baadhi ya askari polisi Kituo cha Polisi Buguruni, wanadaiwa kuwalinda wezi wa mali zilizoibwa kutoka Kampuni maarufu ya Africaries ya jijini Dar es Salaam na kumuhisisha mmoja wa mfanyabiashara maarufu Bw Alphonce Mlawa.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Morningstar POST, baadhi ya polisi wa kituo cha Buguruni majina tunayo wanadaiwa kuwakamata watuhumiwa wote wa mali za wizi na kuwaachi.

Polisi wa kituo hicho walifanikiwa kuwakamata wezi wote waliohusika kuiba mali za mamilioni ya shilingi kutoka kampuni ya Africaries zikiwemo injini nne za magari ya aina ya Land Cruiser na Coater na kuwaachia bila kuwafikisha mahakamani.

Mtoa habari hizi alisema kuwa kesi ya wizi ilifunguliwa kituo cha polisi Buguruni baada ya kufanyika kwa wizi wa injini nne za magari, viyoyozi (IC) sita zenye tamani ya mamilioni ya shilingi.

Aliongeza kuwa mtuhumiwa wa kwanza kukamatwa alikuwa kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Gunda ambaye alimtaja mfanyabiashra maarufu ambaye alikuwa akinunua mali hizo Bw Alphonce Mlawa ambaye  pia alikiri kumfahamu kijana huyo mbele ya polisi.

Hata hivyo polisi baada ya kumkamata mfanyabiashra huyo zaidi ya miezi kadhaa mpaka sasa kesi hiyo haijafikishwa mahakamani. Bw. Mlawa alipoulizwa na Morningstar POST kuhusu habari hizo alijitapa kuwa ziandikwe bila kutoa maelezo yoyote.

Juhudi za kumpata Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Mliro kuzungumzia kesi hiyo hazikufanikiwa mara moja lakini juhudi hizo za kumpata zinaendelea.