Mmiliki wa kampuni maarufu ya ulinzi Bw. Mustaquim Darugar ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kisutu ulioko katikati ya jiji la Dar es Salaam, amemtisha mwandishi wa habari kwa maneno ili asihoji chochote kuhusu kampuni yake na kujitapa kuwa yeye yuko kwenye serikali (yuko kwenye system).

Akizungumza ofisini kwake kwa majigambo na vitisho kwa mwandishi wa habari hizi kutoka Morningstar Post mkurugenzi huyo wa kampuni ya Thinkx GSM Security, alisema yeye yuko kwenye system na jina lake liko Ikulu hatishwi na chochote.

"Mimi niko kwenye system hata nikipiga simu kama na wasiwasi na wewe unakuja sasa hivi kuhojiwa hapa wewe...nataka kupambana na wewe hujui kitu" alisema bw Darugar kwa majigambo.

Alisema katika majina ya wahindi yaliyoko Ikulu jina lake lipo anafahamika hivyo mwandishi wa habari hizi hawezi kumbabaisha kwani yeye ni mtu mkubwa na kiongozi.

Bw Darugar aliyasema hayo baada ya mwandishi wa habari hizi kutaka kupata ufafanuzi wa tuhuma zinazohusu kampuni yake ya ulinzi inayojishughulisha kufungu alarm system.

Hata hivyo Morningstar POST inaendelea kuchunguza tuhuma hizo na uhalali wa bw Darugar kuwepo kwenye system kama kigezo cha kuwa juu ya sheria.