
Mamlaka ya Mapato Nchini TRA, imelalamikiwa kushindwa kushughulikia taarifa za wakwepa kodi zinazotolewa kwenye Mamlaka hiyo.
Maafisa wa TRA kitengo cha kodi za ndani wametupiwa lawama kali kushindwa kutoa taarifa na kushughulikia taarifa za ukwepaji kodi.
Wakizungumza na Morningstar Post, watoa taarifa hao ambao wameomba majina yao yahifadhiwe, walisema kuwa wametoa taarifa za ukwepaji kodi mara kadhaa lakini hakuna majibu ya kulidhisha.
Walisema walitoa taarifa za kukamatwa kwa vitenge vilivyoingizwa nchini bila kulipia ushauri kwenye ghorofa mtaa Nyamwezi Kariakoo mwaka jana, lakini hakuna mrejesho.
Akaongeza kuwa maafisa hao wa TRA walipewa taarifa za ukwepaji wa kodi wa luninga zaidi ya 500 maeneo ya Ilala ambazo TRA wameshindwa kutoa maelezo ya kueleweka kwa watoa taarifa.
"Tulitoa taarifa za ukwepaji wa kodi mafuta ya kula zaidi ya dumu 900 maeneo ya Tabata St. Mary's lakini taarifa zote hizo tunaambiwa ziliingiliana na kitengo cha Investigation" walisema.
Walisema taarifa zote zimetolewa zaidi ya miezi sita lakini tunaambiwa taarifa ziliingiliana na watu wa idara ya uchunguzi.
Watoa taarifa hao wanahoji kama TRA walikamata bidhaa za ukwepaji kodi inakuwaje waambiwe zimeingiliana na idara ya uchunguzi.
Mkurugenzi wa Idara ya Walipa Kodi, TRA, Richard Kayombo alipoulizwa kuhusu habari hizi alishindwa kutoa maelezo zaidi na kuahidi kutoa taarifa hizo baadae.
0 Comments