Mmiliki wa yadi ya magari iliyoko Kurasini jijini Dar es Salaam, Bw. Al-Noor Gulam Husein, amekanusha kuhusika na wizi wa kontena la mifuko (hangers bags), lililokuwa linasafirishwa kwenda Lubumbashi nchini Kongo.
Akizungumza na Morningstar Post kwa njia ya simu, Bw. Gulam alikiri kutokea kwa tukio hilo la wizi wa kontena na kulitupia lawama Jeshi la Polisi Kanda Malaamu ya Dar es Salaam kwa kumuhusisha mtoto wake Samir Al-Noor Gulam Husein.
Alisema baada ya tukio hilo polisi walimkamata Samir na afisa wake mwingine mwandamizi Alex Sanga na kujumuishwa na watuhumiwa wengine 14 katika kesi namba 67 ya 2019 ilifunguliwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Bw. Gullama alisema kuwa waliohusika katika wizi wa kontena hilo walikuwa wanajulikana lakini hawakuhusishwa katika kesi hiyo na kufikikishwa mahakamani.
"Ndugu mwandishi wa habari gari lililosafirisha linajulikana, kwa sababu limesajiliwa na idara ya forodha,
kampuni ya 'clearing' inajulikana kesi ina lundo la watu hatujui hata wametokea wapi akiwemo mtoto wangu, polisi wamemtesa bure", alisema Bw Gulam.
Akaongeza kuwa polisi walimuhusisha mtoto wake katika kesi na mfanyakazi wake bila kufanya utafiti wa kutosha kwa sababu walisema kontena lililetwa kwenye yadi yake ya magari kurasini kitu ambacho sio sahahi kwani hajawahi kuliona kontena hilo.
Alisema kuwa walimuhusisha mtoto wake baada kutajwa na afisa wake aliyekamatwa na polisi kuhusiana na kontena hilo ambalo lilitakiwa kusafirisha kuelekea Lubumbashi nchini Kongo ambako ndiko lilipoagizwa.
Hata hivyo amewataka polisi wawatafute watu wote waliohusika ki ukweli na kulipa milioni 110, 146, 799.00 ambazo ndio kodi ambayo serikali ingeweza kupata kutokana na kontena hilo.
Kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali ambazo Morningstar Post imezipata kuhusiana na sakata la wizi wa kontena hilo, zinaonesha kuwa kontena hilo lililoagizwa na Monga Musodi Gay wa Lubumbashi nchini Kongo mwaka 2019 halikufika nchini Lubumbashi na kuishia hapa nchini kinyume na sheria za mapato.
Kontena hilo liliingizwa nchini na kampuni ya Weifang Zengulu Plastic Co. LTD ya nchini China na kushughulikiwa na kampuni ya wakala wa forodha ya Cargo Conveyors Ltd ambayo mkurugenzi Roselyn Kerand amehusishwa katika kesi hiyo kama mtuhumiwa namba moja ambaye alikaa mahabusu muda mrefu na kampuni yake imefungiwa kujihusisha na shughuli za forodha.
Kwa mujibu wa nyaraka za Mamlaka ya Mapato TRA, kontena hili lilikuwa na mifuko lenye kumbukumbu namba TZDLl191055600 lilitakiwa kupelekwa Lubumbashi nchini Kongo lakini liligeuzwa na kuishia hapa nchini na kutoweka.
Wengine waliohusika katika kesi hiyo ni Geofray Kayanza, Alex Sanga na Hamidu Ali pamoja na Kerand wote waliachiwa huru baada ya kukaa mahabusu kwa muda mrefu.
Hata hivyo tunaendelea kufuatilia sakata hilo kwa upande wa jeshi la polisi ili kujua kama kuna watu wengine waliohusika katika wizi huo ambao wameshakamatwa.
0784663087
0 Comments